Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) Eng. Patrick Mfugale ambaye alikuwa akielezea hatua za ujenzi wa Daraja la JP Magufuli lenye urefu wa Kilometa 3.2 linalounganisha kati ya Wilaya ya Misungwi na Sengerema mkoani Mwanza ambapo limefikia asilimia 27, huku Daraja la kupitisha vifaa likiwa limekamilika kujengwa kwa asilimia 100.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia na wananchi wa Mkuyuni na Butimba Kona mkoani Mwanza wakati akielekea kuzindua miradi mbalimbali ya Maendeleo mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni 2021.
0 Comments