KUAGIZA NA KUSAFIRISHA KWA MELI PITA TASAC KWA ELIMU

Baadhi ya Wafanyakazi wa TASAC wakiwa katika picha ya pamoja.
                                        
Meneja Wakala wa Meli(TASAC) Nelson Mlela akizungumza wakati wa Maonyesho ya Biashara Tanga.

************

Shirika la Wakala wa Meli Tanzania(TASAC)imesema ni vema wananchi wafike kwenye ofisi zao kupata elimu,pindi wanapotaka kusafirisha mizigo yao au kupokea ili wasije wakapoteza wakati wa kusafirisha mizigo yao kwenda nje ya Nchi au kupokea.

Hayo yamesemwa na Meneja Wakala wa Meli(TASAC) Nelson Mlela kwenye maonyesho ya 8 ya Biashara Tanga.

Mlela amesema wakala wa Meli(TASAC)amesema kumekua na changamoto kwenye kuagiza na kupokea mizigo kwa watu wanaoagiza mizigo nje ya nchi na namna ya kupokea,hivyo ni vema wakafika ofisi zao zilizopo Bandari zote hapa nchini.

"Sisi tunatoa maelekezo na ushauri kwa watu,namna ya kusafirisha mizigo yao nje ya Nchi na namna ya kupokea bidhaa zao zinazotoka Nchi mbalimbali kwa maendeleo ya Taifa" alisema Mlela

Ameongeza kuwa katika maonyesho haya wametoa elimu kuhusu usalama  wa maji kwa wasafiri kujua vifaa vinavyotumika Baharini.

"Tumetoa elimu kwa wananchi kuhusu usalama kwa wanaotumia usafiri wa maji,tumewaelekeza kuhusu kutumia life jacketi namna ya kutumia ukiwa kwenye maji"alisema Mlela.

Pia ameongeza kuwa wameongea na walimu waliokuja kwenye maonyesho kuyatumia kuwapa elimu wanafunzi wanaowafundisha,na wawalete kwenye ofisi zao kupata wasaa wakujifunza mambo ya bandari .

"Tumewataka walimu wawalete wanafunzi kuwatembeza kwenye Bandari zote Nchini ili wajifunze shughuli za Bandari,ili wanafunzi waweze kujifunza kuendesha meli,kwa maana ya kuwa Nahodha na kufanya kazi mbalimbali hata kuwa wahandisi wa Meli"alisema Mlela.

Post a Comment

1 Comments