SUUKI KUHAMASISHA UTALII KIMKAKATI

Mshauri mkuu wa Shirika la Urithi wa Utamaduni wa Kiswahili(SUUKI) Dk.Joseph Hokororo akikabidhi mpango mkakati wa Shirika hilo kwa Kamishna Msaidizi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani Ephrahim Mwangomo,uliozinduliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Dk.Hassan Abbasi mwishoni mwa mwaka jana,kushoto ni Mkurugenzi wa SUUKI Joseph Andrew.

Picha ya Pamoja Kamishna Msaidizi akiwa na wajumbe wa SUUKI

Picha ya pamoja wajumbe wa SUUKI

****************
Shirika la Urithi wa Utamaduni wa Kiswahili(SUUKI) wametakiwa kutumia Utalii wa Utamaduni kama njia mojawapo ya kuwavutia wageni wanapokuja nchini ili waweze kuvutiwa na aina mbalimbali za utalii watakaoukuta.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Kamishna wa Uhifadhi katika Hifadhi ya Taifa Saadani, Ephrahim Mwangomo alipotembelewa na Shirika la Urithi wa Utamaduni wa Kiswahili(SUUKI)  walipotembelea hifadhi ya Saadan.

Mwangomo ameeleza kuwa kuna hazina kubwa ya Utalii wa Utamaduni ambao ikitumika vema inaweza kuwa fursa ya kuendeleza Utamaduni hapa nchini.

"Watalii wanaotoka nje ya Tanzania kuja kutembelea Kuna vitu vingi wanavisikia na kikubwa ni Utu wa mtanzania hivyo wanakuwa na Ari ya kujua kuwa yanayosemwa yapo"alisema Mwangomo

Aidha ameeleza kuwa Rais Samia Suluhu ameshafungua anga ya utalii kwa Royal Tour hivyo iliyobaki ni kutekeleza kwa vitendo Yale yaliyotangazwa na Rais kuwa yapo

"Mh Rais Samia Suluhu ameamua kufungua anga la Tanzania kuwa mambo yapo Tanzania,Sasa Kila kitu kipo tayari,Sasa kilichobaki ni sisi kuendeleza hazina kubwa ya utalii wa utamaduni ambao ukitumiwa vizuri itakua fursa ya kuendeleza Utamaduni wetu wa lugha ya kiswahili,ndani ya miaka 50 hizi lugha zingine zote zitafutika,kwa sababu makabila tayari yameshaingiliana hivyo itabaki kiswahili pekee."alisema Mwangomo

Kwa upande wake Mkurugenzi wa SUUKI,Joseph Andrew amesema malengo yao ni kutoa elimu kwenye shule na baadae kuwapeleka wanafunzi kwenye vivutio vya utalii wajifunze zaidi.

"Jambo kubwa ambalo tutatumia kuhamasisha utalii wa ndani tutatumia lugha ya kiswahili ambao utainua utalii kwa haraka sana na watatumia vikundi vya aina mbalimbali kuhamasisha"alisema Andrew

Aidha kwa upande wake mshauri wa SUUKI Dk.Joseph Hokororo ameeleza kuwa utalii unahitajika kutangaza na watu wanaotakiwa kutangaza isiwe kwa Hifadhi tu Bali kwa watu wote ambao wanaweza kutumia utalii kama fursa lakini hapohapo wakiwa wanahamasisha utalii wa ndani.

Nae katibu Mtendaji wa SUUKI Mukumuna Salim ameeleza kuwa utalii zaidi wamelenga kwenda kwa vijana zaidi kwani vizazi vya sasa Utamaduni umekuwa haupo sana kwao,hivyo wao watakua wanapita kutoa elimu na kuwapeleka kwenye sehemu mbalimbali zenye utalii na mambo ya utamaduni ambao kama isipokua endelevu basi vizazi vijavyo kuna baadhi ya mambo yaliyopo kwenye Utamaduni vitakua vimesahaulika.

Mwishoni mwa mwaka jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alifanya Utalii wa Royal Tour ikiwa ni mahsusi kwa nchi ili kuwavutia wawekezaji wa utalii na watalii kuja kujionea Utamaduni halisi wa kitanzania.

Post a Comment

2 Comments