INSTAGRAM MWAMBA AJIFANYA MKUU WA MKOA WA MBEYA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Warren Max Mwinuka (20)Mkazi wa Makondeko,Mbeya Mjini kwa tuhuma za kujifanya Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera akitumia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Instagram kwa jina la“juma homera”.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 07.06.2022 majira ya saa 08:00 mchana huko maeneo ya Mama John Jijini Mbeya. 

Mtuhumiwa alikuwa akitumia akaunti hiyo kuwaadaa watu kwa kujifanya ni Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na kutoa namba ya simu yake ili wananchi waweze kutoa,kupeleka kero,shida mbalimbali kwake.

 Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika atafikishwa mahakamani.

Post a Comment

1 Comments