AL SHABAB WASHAMBULIWA NA VIKOSI VYA MAREKANI

Wanamgambo na Wanachama 10 wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab wameuawa na mamlaka ya kijeshi ya Marekani  ambapo vikosi vya kijeshi vilifanya shambulizi la anga kusini mwa Somalia na kuwaua 

Kundi la Al-Shabaab lenye mafungamano na Al-Qaeda limekuwa likiendesha uasi wa umwagaji damu dhidi ya serikali ya shirikisho dhaifu ya Somalia kwa zaidi ya miaka 17.

Uvamizi huo ulifanyika mnamo Desemba 31 huko Beer Xaani,takriban kilomita 35 kutoka mji wa bandari wa Kismayo

"Tathmini ya awali ya baada ya shambulio ilionyesha kwamba shambulio la anga liliua wanamgambo 10 wa Al-Shabaab huku hakuna raia aliyedhurika," ilisema.

Shambulio hilo dhidi ya Al-Shabaab linafuatia shambulio la kundi la waasi kaskazini mwa nchi hiyo, ambalo lilitimuliwa na vikosi vya serikali.

Al-Shabaab walifanya mashambulizi mengi katika mji mkuu Mogadishu na maeneo mengine ya nchi mwaka jana, huku serikali ikiendelea na mashambulizi yenye lengo la kuwaangamiza magaidi hao.

Post a Comment

0 Comments