Akiwa katika banda hilo Balozi Dkt.Batilda amefahamishwa kuhusu vifaa vinavyoweza kusaidia wananchi kufuatilia na kutambua hali zao za kiafya wakiwa nyumbani, hatua inayoweza kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya.
Amesema ubunifu na matumizi ya teknolojia ni sehemu muhimu katika dunia ya sasa, hivyo ni lazima kuendelea kuwekeza katika maeneo hayo ili kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050.
Balozi Dkt.Batilda amesema bunifu zinazofanywa na vyuo na taasisi za utafiti nchini zina umuhimu mkubwa kwa kuwa zinaweza kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Ameeleza kuwa ubunifu katika sekta ya afya unapaswa kupewa kipaumbele zaidi kutokana na umuhimu wake katika kurahisisha upatikanaji wa huduma na kuwasaidia wananchi kufahamu hali zao za kiafya kwa wakati.
Ametoa wito kwa wataalamu, wanafunzi na taasisi za elimu kuendelea kubuni teknolojia na vifaa vinavyolenga kutatua changamoto za jamii, huku akisisitiza umuhimu wa bunifu hizo kufanyiwa kazi ili ziweze kutumika kwa manufaa ya wananchi.


0 Comments