UMAHIRI WA WAHITIMU WA VETA WANG'ARA WIKI YA VIJANA SUMBAWANGA



Banda la Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) limekuwa kivutio katika Maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Nduwa, mjini Sumbawanga, mkoani Rukwa, kutokana na umahiri wa vijana wahitimu na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya VETA, hususan wenye ulemavu, wanaoonesha ujuzi walioupata kupitia mafunzo ya ufundi stadi.

Maonesho hayo yaliyoanza Oktoba 8 na yanayotarajiwa kuhitimishwa Oktoba 14, 2026, yanafanyika chini ya kaulimbiu “Mazingira Tofauti, Fursa Sawa kwa Vijana,” ambayo imetafsiriwa kwa vitendo kupitia ushiriki wa vijana wenye ulemavu wanaotumia ujuzi wao kubuni na kutengeneza bidhaa mbalimbali.


Miongoni mwa vijana wanaovutia ni Francis Madanganya, mhitimu wa TEHAMA kutoka VETA Kipawa na Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro, mwenye ubunifu wa kifaa cha kuhifadhi na kusambaza umeme kwa kompyuta mpakato (laptop); Gonsalva Lungu na Riziki Ndumba, wahitimu wa Ubunifu, Ushonaji na Teknolojia ya Nguo kutoka VETA Songea; Imelda Kanyengele, mwanafunzi wa fani hiyo VETA Nkasi; pamoja na Ernest Mashiku Igobeko, mhitimu wa useremala kutoka VETA Tanga ambaye ana ulemavu wa uoni.


Umahiri wa vijana hao umevutia wadau mbalimbali, wakiwemo wawakilishi wa Benki ya CRDB, ambao wamenunua bidhaa zao na kuwachangia fedha kwa ajili ya kukuza mitaji ya shughuli zao. Meneja wa Mahusiano na Taasisi za Serikali wa benki hiyo, Paskalina Diu, amesema wataangalia namna ya kuwawezesha vijana hao kupata mikopo na huduma za kifedha zitakazosaidia kukuza shughuli zao za kiuchumi.


Amesema kupitia CRDB Bank Foundation, benki hiyo ina fursa za kuwawezesha vijana kiuchumi, ikiwemo mitaji wezeshi isiyo na riba, ameeleza kuwa kliniki ya taasisi hiyo itatumika kuangalia namna bora ya kuwasaidia vijana wenye ujuzi wa ufundi stadi kujiajiri na kuendeleza shughuli zao.

Kwa upande wake, Imelda Kanyengele amesema mafunzo anayopata VETA Nkasi yamemwezesha kushona aina mbalimbali za nguo na kutengeneza batiki, akiwahimiza vijana wenzake, hususan wenye ulemavu, kutokata tamaa katika kutafuta elimu na ujuzi utakaowawezesha kujitegemea. Maonesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu

Post a Comment

0 Comments