RAIS DK.MAGUFULI AMEENDA KUTOA POLE KWA MAREHEMU BALOZI JOB LUSINDE.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Julai, 2020 amekwenda kutoa pole kwa familia ya Balozi Mstaafu Job Lusinde aliyefariki dunia tarehe 07 Julai, 2020.

Msiba wa Balozi Mstaafu Lusinde upo nyumbani kwake Kilimani Jijini Dodoma.

Mhe. Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amekwenda nyumbani hapo akitokea Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ambako ameongoza Kikao cha Kamati ya Maadili na Usalama na Kikao cha Kamati Kuu ya CCM.
Akiwa nyumbani kwa Marehemu Balozi Mstaafu Lusinde, Mhe. Rais Magufuli amekutana na Mjane wa Marehemu Bi. Sara Lusinde, ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu ambapo ameeleza kuwa kuguswa na kifo cha Balozi Mstaafu Lusinde na kwamba daima atamkumbuka kwa mchango wake alioutoa akiwa Waziri wa Ujenzi, ushauri wake mzuri na moyo wake wa upendo na ukweli.

Post a Comment

0 Comments