Watu wasiojulikana wamefanya shambulizi la bomu lililolenga kanisa lililotekelezwa kwenye eneo la Makassar ambao ni mji mkuu wa jimbo la Sulawesi Kusini nchini Indonesia.
Afisa wa Uhusiano wa Polisi wa Sulawesi Kusini E Zulpan, alitangaza kuwa tukio hilo lilikuwa shambulizi la kujitoa mhanga kulingana na uchunguzi wa awali.
Meya wa mji wa Makassar Muhammed Ramadhan Pomanto, alisema kuwa hali ya wale waliokuwa ndani kwenye misa ya Jumapili wakati wa shambulizi hilo lililolenga kanisa iko vizuri.
Akitoa wito kwa umma kutotegemea taarifa za kupotosha zisitokana na vyanzo rasmi kwenye mitandao ya kijamii na kuwa watulivu, Pomanto alisema kwamba usalama katika eneo hilo umeimarishwa na uchunguzi unaendelea.
Maafisa wa polisi pia walibaini kuwa uchunguzi unafanyika juu ya sehemu za mwili zilizopatikana katika eneo la mlipuko kutambua iwapo zilikuwa za mshambuliaji au mtu mwingine.
0 Comments