MKUU WA WILAYA YA TANGA ATOA RAI KWA WANANCHI KUJIENDELEZA KIELIMU KUPITIA CHUO KIKUU MZUMBE

Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. James Kaji akikabidhiwa zawadi ya kumbukumbu alipotembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe kwenye maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya elimu, ujuzi na ubunifu yanayoendelea katika viwanja vya shule ya sekondari Popatlal jijini Tanga

Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe.James Kaji akiongea na washiriki wa maadhimisho ya wiki ya elimu, ujuzi na ubunifu wa Chuo Kikuu Mzumbe 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha akisaini kitabu baada ya kuwasili kwenye banda la Chuo Kikuu Mzumbe wakati wa Maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya elimu, ujuzi na ubunifu.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof.William Mwegoha akitembelea banda la chuo hicho 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) Dkt.Erasmus Kipesha(kushoto)akipewa maelezo kuhusu Chuo Kikuu Mzumbe na Afisa Mawasiliano Mwandamizi Bi.Fatna Mfalingundi(kulia) wakati alipotembelea banda la kwenye Maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya Elimu,Ujuzi na Ubunifu. 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu cha Dodoma Bi.Rose Joseph akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Chuo kikuu Mzumbe.

**************

Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mheshimiwa James Kaji amewaalika wakazi wa Mkoa wa Tanga kutembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea kwenye Viwanja vya Shule ya Popatlal Jijini Tanga ili kupata uelewa wa kozi na huduma nyinginezo zinazotolewa na Chuo hicho kwenye maonesho hayo.


Mheshimiwa Kaji ambaye pia ni mhitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe amesema kuwa Tanga ni miongoni mwa Mikoa ambayo haina vyuo vikuu hasa vya Serikali na hivyo maonesho hayo ni fursa adhimu kwa wananchi kutembelea na hasa kutembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe ambacho tayari kimeshapata eneo Wilayani Mkinga kwa ajili ya kujenga Chuo Kikuu ndani ya Tanga kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET)na kuanza huduma mkoani Tanga.
 
Aidha Mheshimiwa Kaji amekipongeza Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuanza taratibu za kufungua Kampasi  katika wilaya ya Mkinga Jijini Tanga na kushauri  kutokana na uhitaji mkubwa wa elimu ya juu mkoani humo Chuo Kikuu Mzumbe kuanza kutoa mafunzo kwenye  majengo ya kupanga hadi ujenzi wa  majengo yao utakapokamilika kwani  wananchi wengi  hasa watumishi wamekuwa wakipata changamoto ya kujiendeleza kutokana na kutokuwepo kwa vyuo vikuu mkoani Tanga huku wengine wakikosa likizo za masomo ya muda mrefu kwa Waajiri wao 

“Nachukua fursa hii kushauri uongozi wa Chuo kuangalia namna ya kuanza kutoa huduma kwa kutafuta majengo ya kukodi kwani katika Jiji letu kuna uhitaji sana kwa wanaotaka kujiunga na Elimu ya Juu” alisisitiza Mheshimiwa Kaji.

Post a Comment

0 Comments