MAINJINIA WA MAJI WAN'GARA SHIMUTA.


Mchezaji wa timu ya Tanga UWASA  Mohamed Mn'gazi hayupo pichani akifunga bao la pili dhidi ya MOI katika mashindano ya SHIMUTA yanayoendelea katika viwanja vya Popatlal,katika mchezo huo Tanga UWASA iliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya madaktari wa MOI.

Ushindi wa leo walioupata Tanga UWASA unakuwa ushindi wa tatu mfululizo katika kundi lao tangu mashindano yaanze.


Mapambano yakiendelea katika kuwania ushindi.
Mchezaji wa Tanga UWASA akijaribu kupiga shuti mbele ya walinzi wa MOI.

Madaktari wa MOI wakipambana kupata goli dhidi ya Tanga UWASA lakini bahati haikuwa yao,mpaka mwisho Tanga UWASA waliibuka na ushindi wa 2-0. 

 Benchi la Ufundi likitoa mawaidha kwa wachezaji wakati wa mapumziko.


Post a Comment

0 Comments