MKWAKWANI B-BALL MABINGWA REDE





Bingwa wa kombe la Five Brothers Rede Competition (FBRC)  msimu uliopita Mwakwani Basket Ball  amefanikiwa kutetea taji hilo kwa mara nyingine baada ya kutoka kifua mbele dhidi ya Tanga kwanza.

Fainali hiyo iliyochezwa katika viwanja vya Ccm  mkwakwani mkoani hapa imefanyika kwa round mbili ambapo raundi ya kwanza ilimalizika kwa  Mkwakwani Basket Ball kupata ushindi wa  alama 4 dhidi ya 3 za mpinzani wake Tanga kwanza.

Raundi ya pili  Tanga kwanza aliukataa uteja baada ya kupambana na kulazimisha kutoka sare ya alama 3-3 ikiwa ni tofauti ya alama moja iliyomfanya Mkwakwani Basket Ball kutawadhwa kuwa bingwa wa mashindano hayo kwa msimu huu wa mwaka 2020/2021.

Mashindano hayo yalizinduliwa rasmi February 7  mwaka huu yazikihusisha timu 11za jiji la Tanga zilizoshiriki katika kinyang'anyiro hicho ambapo yamefungwa wikiendi hii na mstahiki meya wa jiji hilo ndugu Abdulhaman Shiloo  ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi  akiambatana na katibu tawala wa wilaya ya Tanga mjini Bi Faidha Salim.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na kampuni ya  Five brothers yalidhaminiwa na Bank ya NMB tawi la Tanga , Anjari Drinking pamoja na Tanga Fresh  ikiwa ni msimu wa tano tangu michuano hiyo izinduliwe.

Post a Comment

0 Comments