MADIWANI JIJI LA MWANZA WAFANYA ZIARA JIJI LA TANGA

Madiwani wa Jiji la Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja nje ya jengo la Halmashauri ya Jiji la Tanga
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Abdulrahaman Shiloo akizungumza wakati akiwakaribisha madiwani kutoka Jiji la Mwanza.


Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akielezea miradi ambayo ipo na itatembelewa na Madiwa wa Jiji la Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Cornelius Cosntantine akizungumza mambo waliyokuja kujifunza katika Jiji la Tanga.


***********

Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza wamefanya ziara katika Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa ajili ya kuangalia namna wanavyofanya shughuli za miradi ya Maendeleo.

Ziara hiyo itawapeleka kwenye miradi mbalimbali ya Halmashauri ya Jiji la Tanga ambayo ni kati ya Majiji Sita yanayofanya vizuri shughuli zake za maendeleo.

Akizungumza wakati wa ukaribisho Meya wa Jiji la Mwanza,Cosntantine Corneli amesema ziara yao ni kuja kujifunza miradi mbalimbali inavyoendeshwa kama Television ambayo Jiji la Tanga inayo.

"Tunatambua umuhimu wa ziara hii sisi Jiji la Mwanza lengo letu kubwa ni kwa ajili ya kutekeleza usimamizi wa miradi ya mapato,ambapo jiji la Tanga ni kati ya majiji sita ambayo inafanya shughuli zake vizuri sana na ndio sababu kuu ya kufika kujifunza namna wanavyojiendesha"

"Shughuli za uvuvi tumekuwa tukifanya katika wilaya ya Nyamagana lakini tumeona tuje tuangalie namna bora ya wavuvi wanavyofanya shughuli zao,sisi tunaredio lakini tukaibinafsisha ila bado imekua inasuasua na nyie mna tv ila tumeona tuje tujifunze namna mnavyoendesha televisheni yenu"alisema Meya Cosntantine.

Baadhi ya Madiwani wa Jiji la Mwanza 
Baadhi ya Madiwani wa Jiji la Mwanza 
Baadhi ya Madiwani wa Jiji la Mwanza 
Baadhi ya Madiwani wa Jiji la Mwanza 
Baadhi ya Madiwani wa Jiji la Mwanza 
Baadhi ya Madiwani wa Jiji la Mwanza 
Baadhi ya Madiwani wa Jiji la Mwanza 
Baadhi ya Madiwani wa Jiji la Mwanza 
 

Post a Comment

0 Comments