Mkurugenzi wa Casafamilia de Rosetta Irene Almasi akitoa elimu ya madhara ya dawa za kulevya kwa waathirika ili waweze kwenda kupata matibabu katika vituo vya Mati ambavyo vipo kwenye kila Hosptali ya mkoa.
Elimu ikiendelea kutolewa
Dkt.Anita Temu ambaye ni Mratibu wa Afya ya akili mkoa wa Tanga akizungumza na wachuuzi wa Samaki walioko eneo la Deep Sea
Elimu ikiendelea kutolewa
Mkurugenzi wa Casafamilia de Rosetta Irene Almasi akitoa elimu ya madhara ya dawa za kulevya kwa waathirika ili waweze kwenda kupata matibabu katika vituo vya Mati ambavyo vipo kwenye kila Hosptali ya mkoa.
Wananchi wakiendelea kupata elimu.
Waathirika wa dawa za kulevya wamekua na tabia za kukaa pembezoni mwa mji na maeneo yaliyojificha kutokana na hali zao zinavyokua.
Jamii hii imekua ikijiona kama wamekuwa wanatengwa na jamii kutokana na tabia zao ambazo hazieleweki ambazo zinaweza kuleta sintofahamu kwa muda wowote hali inayowafanya wakae mbali.
Casafamilia de Rasetta imeamua kuwafuata walipo na kuwapa elimu namna ya kuacha matumizi ya dawa za kulevya na kwenda kupata tiba katika vituo vya Afya ambavyo vipo kwenye kila Hosptali ya mkoa hapa nchini na imeendelea kutoa elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya kwa watu wanaofanya shughuli za uvuvi baharini.
Idadi kubwa ya waathirika wa madawa ya kulevya ni vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa na wao wameona ni vema kuwapa elimu ili waende kupata tiba waachane na madaw ya kulevya.
Akizungumza na vijana na wafanyabiashara wanaofanya shughuli za uvuvi baharini,Mkurugenzi wa Casafamilia Irene Kaoneka amesema kuna vituo ambavyo vipo,vinawasaidia vijana walioathirika kuachana na matumizi ya dawa za kulevya ambavyo vitawasaidia kuwarejesha kwenye hali zao za kawaida.
Naye Dkt.Anita Temu ambaye ni Mratibu wa Afya ya akili mkoa wa Tanga amewaasa vijana hao kukubali kwa moyo mmoja kutoka kwenye hali waliyonayo na kwenda kupata tiba itakayowasaidia kuwarejesha katika hali yao endapo watapatiwa tiba.
"Tanga inashika nafasi ya Pili kwa kuwa na waathirika wengi wa dawa za kulevya hiyo ni mbaya kwetu,tunataka muachane na hii tabia,na utafiti inaonyesha wengi wanaanza kutumia madawa wakiwa shuleni,hivyo ni vema tahadhari ikachukuliwa kwa kuwafuatilia watoto wetu mashuleni"alisema Dkt.Temu
0 Comments