Wataalamu wa Afya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) Mtaalamu wa Afya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) NHIF Ally Mwakababu
****************
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)imeongeza huduma zake katika kuhakikisha kila mtanzania anatumia Bima ya Afya kwenye Matibabu.
Huduma zilizoongezeka ni pamoja na makundi mbalimbali kuweza kutumia Mfuko wa Bima ya Afya kwenye matibabu katika ngazi zote.
Akizungumza kwenye maonyesho ya Biashara yanayoendelea mkoani Tanga Meneja wa NHIF Ally Mwakababu amesema ndio pekee inayoweza kuwapa Wananchi uhakika wa matibabu
"Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya ndio Taasisi pekee inayoweza kutoa uhakika huduma ya Afya juu ya uhakika wa matibabu,hili ni eneo ambalo unaweza kukutana na wananchi wa aina mbalimbali juu ya matibabu"alisema Mwakababu
Mwakababu amesema kuwa kwa sasa huduma zao zimekuwa kubwa na zimeongezeka kwenye kada mbalimbali.
"Mwanzoni tulikua tunatoa huduma kwa ajili ya watumishi wa serikali kuu,ikaja watumishi wa serikali za mitaa,ikaja mashirika,vyomba vya usalama lakini bado Serikali ikawa inahitaji wananchi ndani ya mfuko wa Bima ya Taifa kama unavyojua huduma za Afya ni ghali"alisema Mwakababu
Mwakababu ameeleza kuwa kwa sasa wameomgeza huduma zaidi ambapo kuna watoto,wakulima walioko kwenye vyama vya msingi(amcos),wafanyabiashara.
Pia Mfuko wa Bima ya Afya inatoa huduma mbalimbali za kupima Afya kama Sukari,BP,kupima,uzito kupindukia na huduma zote ni bure.
Mfuko wa Bima ya Afya imekua na vifurushi ambavyo mwananchi atachagua mwenyewe,ninajali,wekeza, timiza ambapo mteja anachagua mwenyewe kutokana na namna anavyotaka kuhudumiwa.
0 Comments