BANDARI CHAFU WASHUKURU KUWEKEWA MFUMO WA MAJI TAKA NA TANGA UWASA

Moja ya chemba iliyokamilika katika eneo la Bandari chafu
Mhandisi Abdul Ramadhani ni Meneja wa Mazingira kutoka Tanga UWASA
***********
Wakazi wa eneo la Usagara Bandari chafu wameishukuru Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika jiji la Tanga(Tanga UWASA)kwa kuwasaidia kuwajengea upya mfumo wa maji taka ambao ulikua kero kwao kwa muda mrefu.

Adha ya wakazi hao ilianza mara baada ya nyumba hizo kubinafsishwa kwao kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania.

Jina hilo limekuja kutokana na adha ya eneo kukumbwa na kadhia ya maji machafu mara kwa mara kutokana na kuharibika mfumo ya maji ya taka unaosababishwa na taka ngumu.

Wakazi hao wameipongeza Tanga UWASA kwa kuweza kuujenga na kuukarabati mfumo wa maji taka na kueleza kuwa tangu kukamilika kwa mfumo,mambo yamekua tofauti na mazingira yamekua masafi tofauti na zamani ambako ukipita maeneo hayo unakutana na maji machafu yakiwa yanaelea hadi eneo hilo kupachikwa jina la Bandari chafu.

"Unajua hapo awali kabla Tanga UWASA hawajafanya ukarabati hapa palikua panaitwa Bandari chafu,tunawashukuru sana Kwa Sasa tunakula Kwa amani,na hatuwazi kama nzi atavamia chakula"alisema Mkazi wa Bandari chafu

Naye Pili Chedi Chikawe amesema mfumo wa maji taka zamani ulikua haufanyi  kazi lakini Tanga UWASA wamekuja kutengeneza na Sasa kila kitu Kiko sawa na hakuna shida yeyote ya chemba kusumbuasumbua na kuziba hivyo.

Mhandisi Abdul Ramadhani ni Meneja wa Mazingira kutoka Tanga UWASA amesema kuwa walipokea malalamiko ya uchakavu tangu 2018,kuhusiana na miundo mbinu ambayo ilikua chakavu sana kwa wakati huo,na waliombwa wauchukue kuusimamia kwa kuwa nyumba hizo zilikua za Bandari kabla ya kubinafsishwa.

Mtandao wa maji machafu ulikua chini ya wamiliki wa nyumba,baada ya kuona kuna changamoto kwa wakazi hao Mamlaka ikatenga Fedha kwa mwaka wa Fedha 2022/2023,wa ajili ya ukarabati wa miundo mbinu na kuichukua kwa ajili ya usimamizi.

"Katika mwaka wa Fedha uliopita mtandao huu ulikarabatiwa,na ukarabati huu ulihusisha ukarabati wa chemba kubwa ambazo zinapokea maji taka kutoka maeneo haya,pamoja na chemba ndogondogo inayounganisha Bomba na Bomba,na sehemu ambazo Kuna Bomba chakavu kufanyiwa mabadiliko"alisema Mhandisi Abdul

Pia Mhandisi Abdul ametoa Rai kwa wakazi wa maeneo hayo hivyo wanatakiwa kutunza miundo mbinu Kwa kuhakikisha takangumu ambazo hazistahili kuingia kwenye mfumo zinatupwa tofauti.

Post a Comment

0 Comments