TETEMEKO LA RITCHER 6.8 LAIKUMBA MOROCCO



Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.8 kwenye kipimo cha Richter limepiga katikati mwa Morocco, katika eneo la Marrakech,usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi. Tetemeko hili limesababisha vifo na uharibifu mkubwa.

Kitovu cha tetemeko hili la ardhi kinapatikana kusini magharibi mwa mji wa kitalii wa Marrakech,kilomita 320 kusini mwa mji mkuu Rabat. 

Kulingana na Taasisi ya Marekani ya Jiofizikia (USGS). Kituo cha Kitaifa cha Utafiti wa Sayansi na Kiufundi (CNRST) chenye makao yake mjini Rabat,kwa upande wake,kimebainisha kuwa tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa wa nyuzi 7 kwenye vipimo vya Richter na kwamba kitovu chake kilikuwa katika mkoa wa Al- Haousi.

Kulingana na vyombo vya habari vya Morocco, hili ndilo tetemeko la ardhi lenye nguvu zaidi kuwahi kukumba nchi hiyo hadi sasa. 

Kulingana na ripoti ya hivi punde,tetemeko hili la ardhi limesababisha vifo vya watu 296 katika majimbo na wilaya za al-Haous,Marrakech,Ouarzazate,Azilal, Chichaoua na Taroudant

Watu 153 wamejeruhiwa na kulazwa hospitalini, kulingana na chanzo kimoja. Ikinukuu vyanzo vya matibabu,tovuti ya habari ya Médias24 imeripoti idadi kubwa ya watu waliojeruhiwa wamesafirishwa katika hospitali za Marrakech.

Post a Comment

0 Comments