Mkurugenzi wa Bougainvillea group of lodges ya mkoani Arusha inayojihusisha na Utalii wa kulala,Nico Ombay akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye maonyesho ya Utalii Mkoa wa Arusha
*************
Kampuni ya Utalii kupitia huduma za kulala ya Bougainvilla group of lodges imewaomba wa Watanzania kufanya Utalii wa ndani,huku ikieleza kuwa ina nafasi ya kuwapa malazi wageni wa aina zote watakaofika nchini kupata sehemu nzuri ya maladhi.
Mkurugenzi wa kampuni Nicodemus Ombay amewaambia Waandishi wa Habari kwenye maonyesho ya Utalii Mkoa wa Arusha maarufu kama 'KILIFAIR',kuwa kwasasa Utalii wa ndani ni gharama nafuu na wanasehemu ya kuwalaza wageni watakapofika kwenda kutembelea mbuga mbalimbali.
Ombay amesema kampuni yao imejipanga kufanya upanuzi zaidi wa uwekezaji na kuongeza uwanda mkubwa zaidi wa ajira kwa Vijana,kwa kujenga hoteli mbalimbali katika hifadhi tofautotofauti.
"tunaendelea kuongeza uwekezaji wetu kwenye vivutio vingine vikubwa zaidi ukiacha Ngorongoro na Serengeti,tutaongeza zaidi katika maeneo mbalimbali Nchini, lakini pia kubwa zaidi ni ajira kwa Vijana zitaongezeka zaidi" Amesisitiza Ombay
"Sekta ya Utalii inanafasi nyingi sana za ajira kwa Vijana waliosomea mambo ya Utalii,hivyo niwaombe Vijana ambao hivi sasa wanasoma,basi wasiache kusomea masuala ya Utalii lakini pia kwa Wazazi wasiache kuwasomesha Watoto wao hasa wakihitaji kusomea masuala ya Utalii"alisema Ombay
0 Comments