EACOP YAWANUFAISHA WALIOPISHA MRADI KWENYE MAENEO

Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Africa  Mashariki(EACOP)kutoka nchini Uganda hadi Chongeleani -Tanzania umehakikisha wananchi wote waliopisha ujenzi wa mradi huo katika mikoa Nane nchini  wananufaika kwa kulipwa fidia zao ambapo ni waguswa zaidi Elfu tisa.

Akizuzungumza na katika warsha fupi ya uelewa wa mradi huo kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Tanga Afisa mawasiliano wa wa mradi wa Bomba  la Mafuta ghafi kwa upande wa Tanzania Abass Abraham  alisema kuwa mradi huo umezingatia mila na desturi za makabila mbalimbali ya Tanzania katika maeneo yao kwani mpaka Sasa wamepatiwa fidia zao kwa asilimia zaidi ya tisini na tisa.

Abbas pia ameeleza kuwa mradi umeheshimu  mila za makabila mbalimbali ambao waliopisha ujenzi wa Bomba  wamenufaika namradi umepita katika  mikoa nane ambazo ni Kagera,Shinyanga,Dodoma singida Geita,Tanga,Manyara na Tabora ambapo katika mikoa hiyo yote,waguswa ambao wamepewa fidia ya pesa taslim na kujengewa nyumba za kudumu.

Sambamba na hayo amewataka waandishi wa habari kuwa na taarifa sahihi  kuhusu mradi ili kuielimisha jamii kuhusu namna mradi unavyoweza kunufaisha watanzania.

Kwa upande wake Mwenyekiti  Chama cha  waandishi  wa habari mkoa wa Tanga  Bi.Lulu George  amewataka waandishi  kupata habari kwa watu sahihi ambao viongozi wa serikali na viongozi mradi ili kuweza kuwahabarisha Jamii kuelewa fursa zilizopo.

Ameeleza kuwa watu wa mradi wamewaaminini waandishi kuwa watasidia kuwapeleka habari sahihi  kwani wanahabari ndio wanaweza kufika eneo husika  ambapo mradi umefika wapate taarifa sahihi na uwepo kwa mradi huo.

Post a Comment

0 Comments