BUNGE LA KENYA KUCHUNGUZA WALIOPENDEKEZWA KUWA MAWAZIRI

Kamati ya Bunge inayohusika na uteuzi inahoji watu 22 walipoendekezwa na Rais inafanya mahojiano watu 22 waliopendekezwa na Rais Wiliam Ruto kuunda Baraza lake la Mawaziri, akiwemo na Mwanasheria Mkuu.

Bunge la Kenya limeanza kuwahoji na kuwachunguza wateuliwa kwenye Baraza la Mawaziri lililotangazwa hivi karibuni.

Rais William Ruto amependekeza majina ya watu 21 wanaotegemewa kuongoza Wizara mbali mbali, akiwemo na Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo.

Kamati hiyo inaongozwa na Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetangula ambapo amesema tunapoanza vikao vya kuidhinisha Wateule wa baraza la mawaziri,ninataka kuwahakikishia wananchi wa Kenya kwamba Kamati ya Uteuzi itachunguza kwa kina kila wasilisho lililotolewa," alisema Wetangula.

"Endapo mawasilisho yaliyopokelewa hayako katika mfumo wa hati za kiapo kama inavyotakiwa kisheria, kamati, kadiri inavyowezekana itajumuisha hoja kupitia maswali kwa wateule," spika huyo ameongeza.

Post a Comment

0 Comments