Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imemaliza hatua ya makundi ya mashindano hayo katika nafasi ya tatu ya Kundi B, nyuma ya Nigeria na Tunisia.
Taifa Stars ilianza kampeni yake kwa kipigo dhidi ya Nigeria katika mechi ya ufunguzi, kabla ya kutoka sare katika michezo miwili iliyofuata dhidi ya Uganda na Tunisia. Licha ya kutopata ushindi wowote na kumaliza na alama mbili pekee, Tanzania imefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora kama moja ya timu nne bora zilizomaliza katika nafasi ya tatu.
Kutokana na kufuzu huko, Tanzania sasa itakutana na wenyeji wa mashindano, Morocco, katika hatua ya 16 bora.
Katika msimamo wa makundi, Tanzania ilimaliza na idadi sawa ya alama na Angola iliyokuwa nafasi ya tatu katika Kundi B, tofauti ikiwa ni idadi ya mabao, ambapo Taifa Stars ilifunga bao moja zaidi.
Kiungo Feisal Salum ameibuka kuwa shujaa wa Taifa Stars na mashabiki wa soka nchini baada ya kufunga bao la kusawazisha katika dakika ya 48 dhidi ya Tunisia kwa shuti kali lililoiwezesha timu kuendelea kuota ndoto ya kusonga mbele.
Hatua hii inaingia kwenye historia ya soka la Tanzania, ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kufuzu hatua ya mtoano baada ya kumaliza nafasi ya tatu. Haya ni mashindano ya nne kwa Taifa Stars kushiriki tangu ilipoanza kushiriki michuano hiyo.
Tanzania pia itakuwa mwenyeji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027 kwa kushirikiana na Kenya na Uganda, hatua ambayo itafanya michuano hiyo kuchezwa Afrika Mashariki kwa mara ya kwanza tangu ilipofanyika Ethiopia mwaka 1976.

0 Comments