Kabudi Akutana na Mjumbe Maalum wa Jumuiya ya Madola Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Profesa Palamagamba Kabudi, amekutana na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Lazarus Chakwera, jijini Dar es Salaam Aprili 9, 2026.

Mjumbe huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi inayolenga kukutana na wadau mbalimbali, ikiwemo viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, asasi za kiraia pamoja na viongozi wastaafu.

Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo inayotarajiwa kukamilika Aprili 16, 2026, Chakwera atatembelea pia miji ya Dodoma na Zanzibar kwa ajili ya mazungumzo na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Chakwera aliwasili nchini Aprili 8, 2026 na kupokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe.

Baada ya kuwasili, alianza ziara yake kwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Aprili 9, 2026 jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Jumuiya ya Madola pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Post a Comment

0 Comments