NDEJEMBI: SITAWAZINGUA WANA WALA SITAMZINGUA MAMA

 MOSHI, KILIMANJARO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amewasihi wananchi wa Mbuyuni, Wilaya ya Moshi, kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na yeye ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo leo, Septemba 1, 2026, wakati akiwasalimia wananchi wa Mbuyuni waliokusanyika kumlaki akiwa katika ziara binafsi mkoani Kilimanjaro.

Amesema kupitia maombi ya wananchi, ataweza kupata hekima na nguvu ya kumsaidia kwa utii Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza majukumu ya kuwatumikia Watanzania.

Mhe. Ndejembi amesisitiza kuwa ataendelea kutekeleza wajibu wake kwa uadilifu, umakini na kujituma, huku akieleza utayari wake wa kushirikiana na viongozi pamoja na wananchi katika kutekeleza majukumu yake.

Akizungumza kwa msisitizo, Makamu wa Rais amesema:

“Hatawazingua Wana wala hatamzingua Mama.”

Amesema kauli hiyo aliitoa pia mkoani Dodoma, kwa wananchi wa Chamwino, mara baada ya kuapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Awali, Makamu wa Rais aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambapo alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa dini pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kilimanjaro.





Post a Comment

0 Comments