Mama Maria Nyerere amewasili mkoani Rukwa kwa ajili ya kushiriki kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru pamoja na Wiki ya Vijana. Akiwasili Rukwa, amepokelewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Rukwa, Sirafu Jumbe Maufi.
Matukio hayo yanafanyika Rukwa yakilenga kuwakutanisha viongozi, vijana na wananchi katika kuadhimisha na kuendeleza ujumbe wa Mwenge wa Uhuru pamoja na nafasi ya vijana katika ujenzi wa taifa.
Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kinatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Nelson Mandela, mkoani Rukwa, tarehe 14 Oktoba, huku Wiki ya Vijana ikiwa sehemu ya shughuli zinazoambatana na maadhimisho hayo.

0 Comments