Basi kama umeshawahi kumshuhudia Karim Benzema wa Real Madrid basi kwa Tanzania ni huyu hapa shujaa wa TRA katika SHIMUTA Maximiliano Maximilian ambaye anacheza mpira huku akiwa ni mfanyakazi wa TRA,wakaamua kumpa jina hilo kwa kuwa anafunga magoli kama Benzema wa Real Madrid.
Mashindano ya SHIMUTA yamemalizika na Timu ya Mamlaka ya Mapato(TRA) imeibuka na Ubingwa wa kwa mchezo wa mpira wa miguu baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa fainali dhidi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika mchezo uliyochezwa katika uwanja wa Mkwakwani.
Shujaa wa
mchezo huo alikua Maximino Maximilian "Benzema" baada ya kufunga magoli mawili kwa timu yake na kutwaa ubingwa wa SHIMUTA kwa
mchezo wa mpira wa miguu.
Akizungumza mara baada ya mchezo shujaa wa mchezo huo Maximino amesema ushindi wao haukuwa mwepesi wameutafuta kwa miaka mingi hadi kuupata.
"Wito wangu kwa wachezaji
wasichoke kupambana kwa timu zote zilizoshiriki kutafuta ubingwa,tumejitahidi
kutafuta ubingwa mwaka jana tulifika fainali tukafungwa kwa matuta,tukarudi
tena takajipanga upya na tumeafanikiwa kuchukua ubingwa".
Kikosi cha TRA kilichotwaa ubingwa wa SHIMUTA katika mchezo wa mpira wa miguu.
Aidha Maxi amewashukuru wenzake kwa hatua waliyoifikia ya kutwaa ubingwa kwa kudumisha upendo,tumedumisha ushirikiano na haya mashindano yatawajenga na kuwa wamoja katika kulisogeza gurudumu la maendeleo la Taifa.
Hata hivyo
ametoa wito kwa timu zingine zilizoshiriki katika SHIMUTA kwa mwaka huu kuwa
wasikate tamaa hata kama wamekosa vikombe.
“Wachezaji wa timu zote shiriki wasichoke kutafuta ubingwa wa mashindano haya kwa mwakani,mpaka sisi kuchukua
ubingwa tulisha-toil,tulishafika fainali tukafungwa lakini hatukukata tamaa na
hatimaye tumeuchukua mwaka huu,na wenzangu wa TRA tusichoke kuchukua tena na tena,tusikose
hamu ya kuchukua ubingwa huu tena”Maxi.
Kipa wa timu ya Ngorongoro akijaribu kuzuia mpira kuingia nyavuni baada ya kupigwa na Maximino hayupo pichani na kuandika goli la pili kwa timu ya TRA.
Mashabiki wa timu ya TRA wakishangilia mara baada ya timu yao kupata goli la pili dhidi ya Ngorongoro.








0 Comments