Diwani Ngamiani Ahamasisha Umoja na Msaada kwa Wahitaji Eid

Diwani wa Kata ya Ngamiani Kaskazini, Fahadi Rished, amewataka wananchi kuendeleza umoja ulioonyeshwa wakati wa Swala ya Eid kwa kuendelea kushikamana na kuwasaidia ndugu na jamaa wasiojiweza.

Akizungumza mara baada ya ibada hiyo, Rished alisema kuwa mshikamano huo ni muhimu katika kujenga jamii yenye upendo na kujali watu wenye uhitaji, hasa katika kipindi hiki cha sikukuu.

Aidha,alibainisha kuwa kata ya Ngamiani Kaskazini ipo katika hali ya usalama, hivyo wananchi wanapaswa kusherehekea Sikukuu ya Eid kwa amani na utulivu bila hofu yoyote.

Alisisitiza umuhimu wa kudumisha amani hiyo kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha sikukuu inaisha salama kwa kila mwananchi.

Post a Comment

0 Comments