WABUNGE WAPIGANA BUNGENI-GHANA

Wabunge wa Ghana, ambao walichaguliwa hivi karibuni wamepigana bungeni baada ya kukosa kukubaliana namna ya kumteua spika.

Chanzo cha ugomvi ni uchaguzi wa spika ambao ulikuwa umepangwa kufanyika kwa njia ya siri, lakini wabunge kutoka chama kinachotawala cha New Patriotic NPP, walikuwa wakionyesha hadharani waliyempigia kura, jambo ambalo liliwakera wabunge wa upinzani.

Wakati utaratibu wa uchaguzi ukiendelea,mbunge wa chama kinachotawala alichukua karatasi za kupigia kura kwa lazima na hivyo kuzua mgogoro.

Polisi wenye silaha na wanajeshi waliitwa bungeni ili kurejesha utulivu.

Chama kinachotawala na upande wa upinzani, wana idadi sawa ya wabunge. Kuna mbunge mmoja asiyekuwa na chama cha kisiasa.

Mahakama ilimzuia mmoja wa wabunge wa upinzani kushiriki katika kura hio ya kujaza nafasi ya spika, baada ya kesi kuwasilishwa mahakamani kupinga ushindi wake katika uchaguzi mkuu. Mbunge huyo hata hivyo alikubaliwa na bunge kushiriki uchaguzi huo.

Wanasiasa wa upinzani wamedai kuwepo udanganyifu katika uchaguzi wa mwezi Desemba na wamewasilisha kesi katika mahakama ya juu kabisa kutaka uchaguzi wa urais kufutiliwa mbali.

Post a Comment

0 Comments