MHE.RAIS SAMIA SULUHU ALIVYO-ONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA HAYATI DKT.JOHN POMBE MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la Hayati Dk.John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania katika mazishi yaliyofayika kwenye makaburi ya familia Chato mkoani Geita 26/03/2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitia Udongo kwenye Kaburi wakati wa Mazishi ya aliyekuwa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli yaliyofanyika March 26,2021 katika Makaburi ya Familia Kijijini kwake Chato Kilimani Mkoani Geita.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la Hayati Dk.John Pombe Magufuli mara baada ya mazishi yaliyofanyika nyumbani kwake Chato mkoani Geita 26/03/2021.

Mama Janeth Magufuli mjane wa hayati Dk.John Pombe Magufuli akikabidhiwa Shada la maua ili kuweka kwenye kaburi la mumewe katika mazishi yaliyofanyika kwenye eneo la familia nyumbani kwake Chato 26/03/2021. 

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Hayati Dk.John Pombe Magufuli mara baada ya mazishi yaliyofanyika nyumbani kwake Chato 26/03/2021.

Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Bashiru Ali Kakurwa akiweka shada la maua katika kaburi la Hayati Dk.John Pombe Magufuli mara baada ya mazishi yaliyofanyika nyumbani kwake Chato mkoani Geita 26/03/2021.
Watoto wa Hayati Dk.John Pombe Magufuli wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao katika mazishi yaliyofayika kwenye makaburi ya familia Chato mkoani Geita


Post a Comment

0 Comments