UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA UGANDA HADI CHONGOLEANI KUANZA MWEZI HUU

Waziri wa Nishati Merdad Kalemani amesema ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima Uganda mpaka Chongoleani Tanga,utekelezaji wake wa ujenzi utaanza Mwezi huu wa nne kwa muda wa miaka mitatu ambapo awali ulikua uanze mwezi wa saba.

Waziri Kalemani ameyasema haya leo 12/04/2021 Bungeni baada ya kujibu swali la Mbunge wa Kiteto Edward ole Lekaita alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kuhusu wananchi kunufaika na fursa za mradi wa Bomba la Mafuta.

Waziri Kalemani amesema awali mradi huo ulikua uanze ujenzi wake mwezi julai mwaka huu lakini baada ya kuweka saini jana na Mh.Rais Samia Suluhu nchini Uganda.

"Utekelezaji wa mradi huu Mh spika na wabunge na watanzania kwa ujumla unaanza mwezi huu,tulipanga kuanza mwezi julai kama tulivyoeza kwenye jibu la msingi lakini tunaanza rasmi mwezi huu kwa muda wa miaka mitatu"

Aidha ameeleza kuwa alishiriki katika zoezi la utiaji saini na Mh Rais Samia Suluhu nchini Uganda katika utekelezaji wa mradi huu jana.

Ameongeza kuwa mradi huu ni mkubwa ambao utapita katika mikoa 8 ,wilaya 24,vijiji 127 na vitongoji 502 na utatoa ajira 10000 katika hatua za awali na hadi ajira 15000 katika shughuli za ujenzi na shughuli za kawaida.

Waziri Kalemani pia akawataka wananchi wa maeneo ambayo mradi utapita wajitokeze kuchukua hizi fursa kwa sababu zimewekwa rasmi kwa ajili ya watanzania.

Post a Comment

0 Comments