KUSUA KWA MIRADI WAZIRI UMMY AMSIMAMISHA KAZI MHANDISI


Ujenzi wa mradi wa Stendi ya Mabasi Mwenge jijini Dar es Salaam ukiwa umesimama kutokana na sababu mbalimbali ambazo zimefanya kukwamisha mradi  huo kukamilika kwa wakati.

******************

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) Mhe.Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi mhandisi Isack Mpaki anaesimamia miradi mitatu ya manispaa ya kinondoni ikiwemo Ujenzi wa Stendi ya Mabasi mwenge, Ujenzi wa Uwanja wa Mpira Mwenge na Ujenzi wa Jengo la Utawala la Manispaa ya Kinondoni baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa mradi huo.

Waziri Ummy amechukua hatua hiyo leo Juni 20, 2021 mara baada ya kutembelea ujenzi wa mradi wa Stendi ya Mabasi Mwenge Jijini Dar es Salaam ambapo ujenzi huo unajengwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa mfumo wa Local Fundi ( Force Account) ulianza Aprili mwaka mwaka jana ambapo pamoja na mambo mengine utaiwezesha Manispaa kukusanya mapato.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mradi huo Waziri Ummy amesema kuwa ili aweze kujiridhisha ni lazima kuundwe timu ambayo itaweza kuchungunza ujenzi wa mradi huo ili aweze kutoa tmko rasmina ujenzi ukaendelea.

Waziri Ummy amesema kuwa amepata malalamiko na jumbe nyingi kutoka kwa wakazi wa manispaa ya Kinondoni hususani wananchi ambao walikuwa wanatumia eneo hilo  wakilalamika kusuasua kwa ujenzi wa stendi ya mwenge ya mabasi ambao ulikuwa umalizike Mei 2 mwaka huu.

Mh.Ummy amechukua maamuzi hayo leo baada ya kufanya ukaguzi na kugundua kasoro mbalimbali kwenyevmiradi hiyo hususani kituo cha mabasi Mwenge ambacho gharama zake za ujenzi ni Bilioni 4.8.

"Nikimsikiliza Mkurugenzi kuna kitu kinaitwa dharau kwa Mkurugenzi wako, haiwezekani Injinia wa Manispaa unaelekezwa na Mkurugenzi wako kumletea taarifa au kusimamia ujenzi halafu hutimizi majukumu yako, hivyo namsimamisha kazi kuanzia leo tuone utendaji kazi wake”alisema Waziri Ummy

“Kuna figisufigisu kwenye huu mradi haiwezekani tukawa tunatupiana mipira kwahiyo  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi Prof.Shemdoe nataka Jumanne aniletee timu huru ya kuja kuchunguza mikataba yote”. Amesema Waziri Ummy.

Post a Comment

0 Comments