Waziri wa Ardhi Anjelina Mabula akizungumza na Waandishi wa Habari.
Dkt.Allan Kijazi Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo na Makazi,akizungumza na watendaji wa Serikali mkoani Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza na watendaji wa Serikali katika mkutano wa Waziri wa Ardhi Anjelina Mabula.Wakuu wa Wilaya za Tanga,Lushoto na Mkinga,Hashim Mgandilwa,Kalisti Lazaro na Kanali Surumbu wakiwa katika mkutano wa Waziri wa Ardhi Anjelina Mabula
Kutoka kushoto mkuu wa wilaya ya Kilindi Abel Busalama akiwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Basila Mwanukuzi kwenye mkutano wa Waziri wa Ardhi Anjelina Mabula.
*************
Akizungumza na Waandishi wa Habari,mara baada ya kufanya mazungumzo na watendaji wa Serikali,Waziri Mabula amesema kuwa,mkoa wa Tanga unavijiji 18 ambavyo vina changamoto na vinne haviwezi kuachiwa,na mengine kufanyiwa marekebisho na kufanyiwa tathmini.
"Mkoa wa Tanga unavijiji 18 ambavyo viko kati ya vijiji 975,kati ya vijiji 18 vijiji 14 vitafanyiwa marekebisho na vijiji vinne kulingana na hali halisi tunavyoiona kama tukiviachia mustkabali wa nchi yetu athari zake itakua kubwa zaidi,kwa hiyo tunakwenda kufanya tathmini kuweza kujua hatma ya vijiji vinne,tutaacha timu hapa itapita katika maeneo wakifanya tathmini na kuja na ushauri kwa serikali hatua za kuchukua"alisema Waziri Mabula
WaziriMabula ameongeza kuwa wao wamefika kutoa maagizo kwa mkoa,na mkoa kufanya utekelezaji wa maagizo ya Baraza la Mawaziri.
"Pamoja na tathmini itakayokua inaendelea mkoa kama mkoa watajipanga katika utekelezaji,sisi tumekuja kuwapa maamuzi ya baraza la mawaziri,ambayo tayari yana baraka za Mheshimiwa Raisi kwa hiyo swala la utekelezaji wanaanzia wapi wanaishia wapi ni jukumu la mkuu wa mkoa na timu yake,rai yangu naitoa kwa mkoa ni ushirikishwaji katika swala la kutekeleza maamuzi ili isitokee mtu kalalamika kaonewa,jukumu letu kama serikali ni kuhakikisha tunatoa elimu ili masuala haya yasijirudie,kwa sababu tukiwa na operesheni mbalimbali ambazo mwisho wa siku utekelezaji au usimamizi wake unakua sio mzuri sana,matokeo yake yanajirudia,sasa kipindi hiki chini ya Mh.Rais Mama Samia Suluhu Hassan,asingependa kuona masuala haya yanajirudia,tunalolitaka ni kila mmoja awajibike na ndio maana nimesisitiza mkuu wa mkoa akiwa na wakuu wa wilaya,maafisa tarafa na watendaji kule chini kila mmoja akisimamia jukumu lake nadhani swala kama hili halitajirudia tena"alisema Waziri Mabula
Waziri Mabula ametoa rai kwa wananchi watakao kuwa wametengewa maeneo na kuwekewa matumizi bora ya ardhi waheshimu maelekezo watakayopewa na washiriki wa zoezi hilo.
"Rai yangu kwa wananchi kwa wale watakao kuwa wametengewa maeneo na kuwekewa mpango bora wa matumizi bora ya ardhi katika maeneo yao, hatutarajii tena waendelee kuingia katika maeneo ya hifadhi ambayo yamezuiliwa,hatutarajii waingie katika maeneo ya vyanzo vya maji,lakini hatutarajii pia kuingia katika maeneo ya taasisi mbalimbali ambayo wamekua wakivamia,maana yake hayo ndio yametufikisha hapa tulipo"amesema Waziri Mabula
Aidha ameongeza kuwa ni vema watendaji wote wa Serikali kila mmoja awajibike kwa nafasi yake ili kuweza kuondoa matatizo madogomadogo yanayoweza kutatulika kwa wakati.
"Kikubwa kila mmoja ana nafasi yake, watumishi wa serikali na watendaji wana nafasi yao ya kufanya usimamizi wa mambo haya yasijirudie,lakini wananchi wanatakiwa kutii sheria bila shuruti,tusingepanda kuona mambo haya yanajirudirudia na kwa wale ambao wanaovamia maeneo na wakitarajia serikali itaridhia waendelee kuwa pale,hii halitajirudia tena"alisema Waziri Mabula
Waziri Mabula ameeleza kuwa zoezi hili la awmu ya pili inayofanyika halitajirudia tena,hivyo ni vema kila mmoja kuti sheria bila shuruti ili kuepuka usumbufu ambao hauna tija kwa jamii.
"Tukishafanya hiki hatutarajii tena kutakua na masuala ya urasimishaji,au kuridhia kumega tena maeneo tunahitaji kila mmoja aweze kutekeleza wajibu wake kwa kutii sheria bila shuruti,hilo ndio kubwa tunalotaka kila mmoja aelewe,maana hatuwezi kufanya zoezi hili kila mwaka"alisema Waziri Mabula.
Waziri wa Ardhi ameendelea na shughuli ya kutatua migogoro ya ardhi katika awamu ya pili katika vijiji 975 ambayo baraza la mawaziri imeridhia kufanyiwa marekebisho na mengine kufanyiwa mpango wa matumizi.





0 Comments