MAGOMENI FC MABINGWA WILAYA YA TANGA




Bao moja pekee la Ibrahim Ramadhani  limetosha kuipa Magomeni ubingwa wa ligi daraja la nne ndani ya wilaya ya Tanga mjini mbele ya Mwadongo FC katika fainali iliyopigwa kwenye dimba la Lamole  mkoani hapa.

Magomeni anaingia kwenye ligi ya mkoa baada ya kufanikiwa kukusanya jumla ya alama 7 pamoja na Makorora Stars ambao walishika nafasi ya pili wakifanikiwa kujikusanyia alama 5 huku Mwadogo akiwa ni watatu akiwa na alama 4 Magomeni yeye akiwa mkiani  bila alama hata moja zote akiishia kuzigawa kwa wenzake.

Akikabidhi kombe hilo mgeni rasmi ambaye ni mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Tanga mjini Kiama Mwaimu aliwataka wachezaji hao kwenda kuiwakilisha vyema wilaya hiyo Katika mshindano ya mkoa huku wakielewa kuwa michezo kwa sasa ni ajira.

"Hongereni kwa ushindi mnakwenda sasa kwenye ushindani wa mkoa mwende huku akitambua kuwa wilaya inawatizama nyie, kwa sasa michezo ni ajira kwahiyo muone thamani ya mpira kwa sasa" alisema Mwaimu.

Nahodha wa mabingwa hao  wa wilaya kwa msimu huu Salimu Bakari alisema walikuwa wanapambana kwa kila hatua wakiamini kuwa lazima wachukue ubingwa huo hatimaye wamefanikiwa wanajipanga sasa kuelekea ligi ya mkoa kwenda kuonyesha upinzani m.

Tunakokwenda ni kugumu zaidi tutujitahidi  tukifuata pia maelekezo ya kocha naamini tutajipanga zaidi kwenda kuonyesha ushindani, mashabiki zetu waendelee kutupa ushirikiano tunaomba pia wadau wajitokeze kutusaidia" alisema

Ligi hiyo imezihusisha timu 34 ambazo zilishiriki katika kinyang'anyiro hicho na hatimaye bingwa amepatikana akimbeba na
Makorora kwenda ligi ya mkoa.

Post a Comment

0 Comments