Meneja wa RUWASA Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo akisaini mkataba wa Usambazaji Mabomba katika wilaya nne za Mkinga,Kilindi,Lushoto na Handeni,kushoto ni Mhandisi wa RUWASA wilaya ya Mkinga Kaijage Thomas na Mwakilishi wa kampuni ya Kahama Mhandisi Alfred Shima.
Usambazaji wa mabomba hayo yatakua katika wilaya za Lushoto,Handeni,Mkinga na Kilindi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wakisaini makubaliano hayo,Meneja wa RUWASA mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo amesema usambazaji wa mabomba hayo utakapo kamilika utawanufaisha zaidi ya watu elfu ishirini ambao watapata huduma ya maji.
"Miradi hii itakapokwenda kukamilika,itaongeza idadi ya watu 28638 katika upatikanaji wa huduma,watu hawa ni Sasa na asilimia 1 ya watu wa Tanga,Miradi hii iki kamilika watu wa Tanga watakua watakua wamepata huduma ya maji saafi na salama,na ya kujitosheleza.
Aidha Mhandisi Upendo ameeleza kuwa ni vema mabomba hayo yafikishwe kwa wakati kama walivosaini kwenye mkataba
"Tunataka mabomba haya yafike kwa wakati,inatakiwa yasambazwe ndani ya siku 30,siku 14 kutoka leo na baada ya siku14 ziwe zimefika eneo la kazi yaanze kufukiwa ili wananchi waanze kupata maji"alisema MhandisiUpendo.
Kwa upande wake Mhandisi wa RUWASA wilaya ya Mkinga Kaijage Thomas amesema mabomba hayo yatakwenda kwenye miradi yake amewataka wananchi wazitunze miundo mbinu ya maji wakati ujenzi ukiendelea na wazitunze ili mradi wa maji iweze kudumu.
Naye Mhandisi Alfred Shima kutoka kitengo cha Uzalishaji na Mauzo kutoka kampuni ya Kahama ambao wanasambaza mabomba hayo amesema maagizo aliyopewa na Meneja wa RUWASA mkoa wa Tanga yatatekelezwa kwa wakati na kuahidi ndani ya siku 14 wataanza kusambaza mabomba hayo.
0 Comments