Wabunge wa mkoa wa Tanga
Mganga mkuu wa Mkoa wa Tanga Jonathan Budenu
*************
Mkoa wa Tanga umepokea kiasi cha shilingi Bilioni 8.9 kuanzia mwezi Julai hadi December kwa ajili ya ujenzi wa Hosptali tatu huku fedha hizo zikiwa katika mgawanyo wa kujenga vituo vya Afya,Zahanati na ukamilishaji wa Hosptali tatu zilizopewa fedha mwanzo.
Akizungumza kwenye kikao cha maendeleo ya Mkoa wa Tanga Mganga mkuu wa Mkoa wa Tanga Jonathan Budenu,ameeleza kuwa fedha hizo zimeingia katika kipindi cha mwezi Julai hadi December mwaka 2021.
"Katika kipindi cha Julai December Mkoa wa Tanga umepokea Bilioni 8.9 kwa ajili ya ujenzi wa hosptali tatu,na fedha hizo zimegawanyika kama ifuatavyo ambapo billion 3.5 ni vituo vya afya,Bilioni 4.9 ni Zahanati na Bilioni 1 kukamilisha ujenzi wa Hosptali tatu zilizopokea fedha mwanzoni,na tuna vituo 17 ambazo zimejengwa kwa fedha za tozo"alisema Budenu
Budenu ameongeza kuwa katika kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kiusawia,Hosptali ya Mkoa Bombo imepokea fedha Shilingi Billioni 6 kwa ajili ya upanuzi wa Jengo la wagonjwa wa dharura na mahututi na tathmini inaonyesha kuwa imepunguza vifo kwa asilimia 70.
"katika majengo ya magonjwa ya dharura kwa mkoa yaliyoongezwa katika hosptali ya bombo imepunguza vifo kwa asilimia 70,sasa majengo yakikamilika wilaya za Korogwe,Mkinga na Handeni vijijini pamoja na Kilindi inaweza kupunguza vifo kwa asilimia kubwa sana zaidi ya hizo"alisema Budenu
Aidha hosptali ya mkoa ya Bombo imepokea kiasi cha shilingi Millioni 400 kwa ajili ujenzi wa kituo cha damu salama ambapo itakua inahifadhiwa hapo hosptali na haitakuwa inapelekwa KCMC kwa ajili ya kufanya screening.
"Tumepokea millioni 400 tunajenga kituo cha damu salama,ambapo itakua haina haja ya kupeleka damu KCMC au Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa screening"alisema Budenu
Ameeleza kwa sasa taratibu za damu salama inachukua muda mrefu ambapo damu ni lazima ipelekwe hosptali ya KCMC kwa ajili ya kufanyiwa screening ambapo wakatti mwingine inachukua muda mrefu kupata majibu.
Naye mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima ameeleza kuwa sekta ya afya inahitaji uwekezaji mwingi katika vifaa ili kuokoa maisha ya watu.
0 Comments