Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza na mmoja wa watoto aliyepo katika vituo vinavyotunza watoto yatima,mbele ni watoto wengine ambao wanalelewa katika kituo alichowapa msaada.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amekabidhi msaada wa vyakula kwa makundi maalumu yenye mahitaji maalumu yakiwemo Wazee wasiojiweza na Watoto yatima.
Akikabidhi
msaada huo,Rc Kindamba alisema Ofisi yake imeona sio jambo zuri
kusherekea sikukuu ya Eid bila kuwakumbuka Watu Wenye Mahitaji Maalumu,
"Tumeona
sio jambo zuri kusherekea sikukuu kwa furaha Wakati Kuna wenzetu
wanahitaji ,tumeamua tuungane kwa pamoja kuhakikisha tunasherekea
sikukuu kwa furaha"alisema Kindamba
Katika
hatua nyengine, mkuu huyo wa Mkoa aliahidi kuzifanyia kazi changamoto
zilizopo kwenye vituo hivyo hususani Kituo Cha lelea Wazee wasiojiweza
Duga ambacho miundombinu yake imechakaa ,
"Sitaki
kuwa msemaji Sana naomba tukazifanyie kazi changamoto hizi ,nimeambiwa
miundombinu ya Umeme ni mibovu ,Majengo pia machakavu na mengine mengi
tutayafanyia kazi" alisema Kindamba
Vituo
vilivyonufaika na msaada huo ni pamoja na Kituo Cha Wazee wasiojiweza
Duga,Kituo cha Watoto yatima Good Will na Kituo cha kulea
Watoto yatima Ansar huku makundi yote yakinufaika na
Mchele,Mafuta,Mbuzi,Maharage na Soda.
0 Comments