Mwenyekiti ya PAC,Mh.Naghenjwa Kaboyoka akizungumza na Mh.Hamisi Kigwangwala pamoja na Mh.Aida Kenani wakati wa ziara ya kamati hiyo kwenye kituo cha izalishaji Umeme Hale.
Afisa wa kituo cha uzalishaji Umeme Hale Kombo S.Kombo,akitoa maelezo ya Lifti kwa Kamati ya PAC,ili kushuka kwenye uzalishaji Umeme
Wafanyakazi wa TANESCO wakiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji Umeme na Huduma kwa wateja kutoka Shirika la Umeme(TANESCO),Mhandisi Athanasius Nangali,baada ya kumalizika kwa kikao.
Wafanyakazi wa TANESCO wakiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji Umeme na Huduma kwa wateja kutoka Shirika la Umeme(TANESCO),Mhandisi Athanasius Nangali,baada ya kumalizika kwa kikao.
*****************
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC)imeagiza kuwaita Dodoma,Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati,Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO na Mwenyekiti wa Bodi juu ya kutoa ufafanuzi wa Mradi wa Umeme wa Hale kama kuna fedha za kuendeleza ukarabati ili Umeme uwe wa uhakika kwa manufaa ya Nchi.
Mitambo ya uzalishaji umeme Hale,inakabiliwa na changamoto ya vifaa kutokana na vifaa vyake vingi kuwa chakavu tangu ilipojengwa mwaka 1964 ndio vinavyotumika hadi leo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo,Mwenyekiti wa kamati hiyo Mh.Naghenjwa Kaboyoka amesema mitambo hiyo ilijengwa vema kwa wakati huo,lakini kwa sasa mitambo ya kisasa inahitajika,ili kuweza kuzalisha umeme wa kutosha.
"Kazi ile inatakiwa ifanyike,na kuna masuala ya fedha,bado hatujahitimisha,kutokana Afisa masuhuli,Katibu mkuu wa Nishati,Mtendaji mkuu wa Tanesco na Mwenyekiti wa Bodi ndio wanaotakiwa kujibu hawapo,kwa hiyo hapo hatujahitimisha,na tumepanga kuwaita Dodoma,kamati hii inataka majibu yanayotoka kwa yule ambaye anayehusika na sio mwakilishi wake.
"Kuna mambo mengine mwakilishi hawezi kuyajibu kwa hiyo tumeahirisha kikao hiki na viongozi wale watapewa barua kutoka bungeni,waje wakutane na kamati hii Dodoma,na viongozi hao watakua Afisa Masuhuli,Katibu Mkuu Wizara ya Nishati,Mwenyekiti Bodi ya Tanesco na Mtendaji mkuu wa Tanesco,hapo ndio tutajua kama Mradi wetu unaweza kuendelea au la kutokana na fedha iliyopo"alisema Mh.Kaboyoka
"Kuna kazi nzuri ilifanyika enzi hizo za mwaka 1964 walipokua wakijenga mitambo,ila Kwa Sasa Kuna hitajika maboresho makubwa ya ukarabati Kwa kuwa tabaini Moja imeharibika"alisema Mh.Kaboyoka
Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji Umeme na Huduma kwa wateja kutoka Shirika la Umeme(TANESCO),Mhandisi Athanasius Nangali ameeleza kuwa ujio wa kamati ya PAC kutembelea kituo cha Uzalishaji umeme Hale,ni mwanzo wa kufanya kituo hicho kuzalisha umeme kwa ubora na kuwa ya kisasa.
"Tunaishukuru kamati ya PAC,pamoja na kuwa na muda mfupi lakini wameweza kutembelea Hale ambayo inazalisha Megawatt 21,ujio wa kamati hii ni kwamba wametembelea na wameona na tunaimani watasapoti juhudi zetu za kuifufua hiki kituo kiweze kufanya kazi kwa ubora zaidi,sasa hivi mpango tulionao nikuifanya kiwe kituo cha kisasa,taratibu za ununuzi ziko mwishoni wa kumpata mkandarasi ili kituo kiwe bora kuzalisha umeme mzuri Kwa manufaa ya Taifa"alisema Nangali.
Kamati ya Bunge na Hesabu za Serikali imetembelea Chanzo cha Maji bwawa la Hale na kituo cha Uzalishaji umeme Hale na namna wanavyotekeleza shughuli zao tangu kituo hicho kilivyoanzishwa tangu mwaka 1964.

0 Comments