KITUO CHA TFF YAMLIPA DIWANI

Diwani wa Kata ya Usagara Michael Mwenda(mwenye Tshirt)akiwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tannzania(TFF)Wilfred Kidao alipotembelea kituo cha kukuza vipaji iliyoko Mnyanjani,Tanga.

Diwani wa Kata ya Usagara Michael Mwenda aliongozana na watendaji wakuu wa Kata yake akiwemo Afisa Elimu Kata kwa Sekondari,Watendaji wa Kata pamoja na Mtaa,wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tannzania(TFF)Wilfred Kidao walipotembelea kituo cha TFF cha kukuza vipaji iliyopo Mnyanjani,Tanga.

Diwani wa Kata ya Usagara Michael Mwenda akitoa zawadi ya mpira kwa Mwalimu wa Shule ya Kombezi baada ya kukamilika kwa ligi ya Mafita Cup.

Diwani wa Kata ya Usagara Michael Mwenda akitoa zawadi  kwa mchezaji bora wa michuano ya Mafita Cup ambapo bingwa ni Timu ya Tanga Football Club.

**************

Diwani wa Kata ya Usagara Michael Mwenda alitembelea kituo cha Michezo cha Shirikisho la Soka Nchini TFF ambayo inajengwa katika eneo la Mnyanjani katika jiji la Tanga ambapo sasa imemlipa baada ya timu yake ya Tanga Footbal Club kutwaa ubingwa ikiwa na wachezaji vijana kabisa chini ya miaka 19.

Katika ziara hiyo Mh.Mwenda aliongozana na watendaji wakuu wa Kata yake akiwemo Afisa Elimu Kata kwa Sekondari,Watendaji wa Kata pamoja na Mtaa wote wakiwa ni viongozi katika kata hiyo.

Lengo kuu ni kujua namna shughuli za michezo zinavyoendeshwa hasa katika kukuza vipaji kwa vijana wadogo ambapo walikutana na Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kadao ambaye walifanya mazungumzo na kuwaeleza namna bora ya kutafuta vijana na kuwatengeneza kuwa katika timu ya ushindani.

Kidao aliwaeleza kuwa kituo hicho kipo kwa ajili ya kukuza vijana ili waweze kuja kuwa wachezaji wazuri katika siku za badae wakipata usimamizi mzuri kutoka katika kituo hicho,pia kutakua kunafanyika michezo mbalimbali kwa ajili ya kutafuta vipaji halisi vya soka.

Mh.Mwenda safari yake ya ziara katika kituo cha TFF,ni kuhakikisha timu yake ya Tanga Football Club,inapita katika njia sahihi ya soka,ambayo itakua inawanufaisha vijana moja kwa moja.

Tanga Football Club wamefanikiwa kuwa mabingwa katika kombe la Mafita lililomalizika mwishoni mwa wiki hii,ambapo mlezi wa vijana hao Mh.Michael Mwenda alifurahishwa na kiwango cha timu yake baada ya kuifunga timu ya United Worries kwa Penati 5-4.

"Baada ya mashindano haya kukamilika na timu imekuwa bingwa katika kipindi kifupi,walivyouchukua ubingwa inanipa hamasa zaidi nani deni kwangu,ambalo na enda kulirejesha kwao"Diwani Mwenda.

Baada ya mafanikio hayo Mwenda amesema kwa sasa atageukia soka la Wanawake katika Kata yake ya Usagara,na tayari ameshaanza mikakati na kabla ya mwaka kuisha ligi ya Wanawake itachezwa katika kata hiyo.

Post a Comment

0 Comments