Penalti Zamrudisha Awesu Awesu Nyumbani

Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Meridianbet Tanzania,Matina Nkurlu akimkabidhi mchezaji wa KMC Awesu Awesu zawadi atakayoigawa katika jamii.

**********

Katika muendelezo wa kuhakikisha inagusa jamii kampuni ya michezo ya ubashiri Meridianbet Tanzania iliandaa utaratibu wa kushirikisha watu maarufu na wenye ushawishi kwenye jamii kushiriki kwenye shindano la mikwaju ya penati ambapo kwa kila penati alipaswa kupata kiasi ambacho matumizi yake yangebadirishwa na kwenda kutoa msaada kwenye jamii yake.

Sehemu ya kwanza ya Shindano hilo ilianza na mchezaji wa KMC Awesu Awesu ambae kiasi kilichopatikana alipendekeza kiende kwenye jamii yake aliyokulia Magomeni jijini Dar es Salaam , sehemu ambayo yeye amekulia na kwa upande wake aliona ni vyema kuiwezesha jamii ya kipato cha chini katika eneo hilo.

Akiongea na wanahabari Awesu Awesu alisema 

"Kwanza nimshukuru mungu kwa kuniwezesha kufikia leo, lakini kubwa zaidi nawashukuru wadhamini wa timu ninayotumikia kwa sasa na imekua faraja sana kwangu kuifikia siku hii na kuifikia jamii inayonizunguka, kwa maana leo mimi ndio kioo cha mtaa wangu na kesho huenda akaibuka mwingine na kuirudishia faraja jamii hii hii iliyotukuza"Alisema Awesu

Kwa niaba ya Meridianbet Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Meridianbet Tanzania, Matina Nkurlu alisema 

"Huu uliofanywa na Awesu Awesu leo ndio Uungwana kwa mana Tafsiri ya uungwana ni pamoja na kujali njia ulizopita na kuzipa faraja,leo Meridianbet tukishirikiana na Awesu Awesu tumefika hapa magomeni kuzipa Faraja familia na wakazi wa wa hapa alipoishi Awesu hadi kufikia ndoto zake za kucheza mpira wa miguu, Na kesho huenda akawa mtu mwingine mkubwa kwenye jamii akafikia pia jamii yake kupitia sisi, kwahiyo lazima tukubali kua huu utakua muendelezo kutoka kwetu Meridianbet kwenda kwa Jamii inayo tuzunguka "

Meridianbet pia wameahidi kuendelea na mchakato wa kuhusisha watu mashuhuri kwenye mashindano ya kimichezo kama penalti na danadana ili kuchangia kiasi  cha fedha kitakachoweza kutumika kwenye kutoa misaada mbalimbali kwenye Jamii.

Post a Comment

0 Comments