Wananchi wa Wilaya ya Ruangwa, Mkoa wa Lindi wameonesha kupongeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan na ujio wake katika Wilaya hiyo umewapa faraja.
Wakazi hao wakizungumza katika nyakati tofauti leo wilayani hapo wamesema kuwa Serikali imeboresha maisha yao kwa kuwafikishia huduma mbalimbali.
Mkazi wa Kilimahewa Wilaya ya Ruangwa, Bi. Rahma Hokororo amesema kuwa ziara ya Rais Samia katika Wilaya Ruangwa inawapa matumaini kuwa miradi mingi zaidi ya maendeleo itatekelezwa kwa manufaa yao.
Bw.Abubakar Mkwepu amesema kuwa waanamini ujio wa Mhe. Rais utawapa fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na wajasiriamali kuuza bidhaa zao na wengine kuona fursa za uwekezaji zilizopo wilayani humo.
"Baadhi ya miradi imekamikika, mfano Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, pia kuna vituo vya afya ikiwemo cha Mbuyuni vimekamilika na tayari vimeanza kutoa huduma kwa kweli tunampongeza na kumshukuru Rais Samia"ameeleza Bw.Mkwepu.
Ameongeza kuwa katika miradi ya elimu, kuna majengo ya kisasa katika kila kijiji na wanafunzi wasoma katika mazingira bora.
Mhe.Rais Samia ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Lindi ambapo ataweka mawe ya msingi na kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Shule ya Sekondari ya Wasichana Lindi,Bandari ya Uvuvi sambamba na kuzungumza na wananchi katika mkutano ya hadhara.
0 Comments