MIRADI 79 KUCHUNGUZWA NA TAKUKURU

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Tanga imeanza kuchunguza miradi minne ya maendeleo yenye thamani ya bilioni 1.1 iliyobainika kuwa na mapungufu wakati wa utekelezaji.

Miradi hiyo ni kati ya miradi 79 yenye thamani ya bilioni 34.5 iliyotekelezwa katika sekta za kipaumbele ambazo ni elimu, barabara, maji na afya.

Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa kipindi cha kuanzia April hadi Juni mwaka huu kwa niaba ya Mkuu wa Takukuru mkoa Tanga Afisa Uchunguzi Mwandamizi wa TAKUKURU mkoa huo Frank Mapunda amesema miongoni mwa miradi hiyo ya maendeleo, miradi minne imebainika kuwa na mapungufu kadhaa iliyopelekea kuanzishwa kwa uchunguzi.

Aliitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya msingi Kisinga wenye thamani ya sh 50.milioni katika Halmashauri ya wilaya ya Lushoto,ujenzi wa zahanati ya Milingano wenye thamani ya sh 553,000,000,upanuzi wa kituo cha afya Mgwashi wenye thamani ya sh 500.milioni na mradi wa zahanati ya Mkaalie wenye thamani ya sh 50,000,000.

Post a Comment

0 Comments