UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJI TAKA-DUGA KUNUFAISHA ZAIDI YA WANANCHI 500

Mradi wa Majitaka Duga Mwembeni unaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (TANGA UWASA) unatarajia kuhudumia zaidi ya wananchi 500 wa Tanga Jiji.


Mradi unatekelezwa na Mkandarasi Irmanos Company Limited chini ya usimamizi wa watalaamu wa TANGA UWASA kutoka kitengo cha Huduma ya Majitaka na mradi upo kwenye hatua za awali ambapo zinajumuisha umwagaji wa zege kwenye kituo cha kusukuma majitaka na unatarajiwa kukamilika Mwezi Aprili,2025.

Mradi una gharama ya Shilingi za Kitanzania Milioni 458 na utekelezaji wake umefikia asilimia 35, ambapo lengo kuu la utekelezaji wa mradi huo ni kuhakikisha majitaka kutoka maeneo ya Duga Mwembeni,Msambweni,Mabawa na makorora yanakusanywa na kusafirishwa katika hali salama na kutunza Mazingira.

Post a Comment

0 Comments