Mahakama ya Kijeshi nchini Uganda imemtia hatiani Eron Kiiza, na kumpa kifungo cha miezi tisa jela mwanasheria huyo wa mwanasiasa Kizza Besigye kwa kukaidi amri ya Mahakama.
Hatua hiyo inakuja baada ya mwanasheria huyo kukamatwa mapema Januari 7, wakati alipokuwa mahakamani kumtetea mteja wake.
Timu ya mawakili wa utetezi 32 wa Dkt Kizza Besigye na Obeid Lutale wamegoma kuendelea na kesi hiyo baada ya mwenzao kutupwa kwenye gereza la Kitalya kwa tuhuma za kudharau mahakama.
Kiiza alipewa hukumu bila kuwepo ndani ya mahakama hiyo ya kijeshi.
Mapema Januari 7,Kiiza alikamatwa ndani ya viunga vya mahakama hiyo, kitendo kilichoibua vurugu kubwa ndani ya eneo hilo, wakati alipokuwa anajiandaa kuhudhuria usikilizwaji wa kesi inayomkabili Besigye na Lutale ndani ya Mahakama ya Kijeshi ya Makindye.
Martha Karua na Erias Lukwago walisisitiza kuwa hawakuwa tayari kuendelea na keshi hiyo bila ya uwepo wa mwenzao, wakisisitiza kuwa alikuwa na “ushahidi muhimu.”
0 Comments