Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Bara, Ndugu John Mongella, leo Januari 17, 2027 amekagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya chama hicho unaoendelea katika eneo la NCC jijini Dodoma.
Katika ukaguzi huo, Dkt. Migiro amepata maelezo kutoka kwa wasimamizi wa mradi kuhusu hatua iliyofikiwa, mwenendo wa ujenzi pamoja na changamoto zinazojitokeza, huku akisisitiza umuhimu wa mradi huo kukamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyokidhi mahitaji ya chama.
Mradi wa ujenzi wa Makao Makuu ya CCM Dodoma unalenga kuboresha mazingira ya kazi kwa viongozi na watendaji wa chama, sambamba na kuimarisha ufanisi wa utekelezaji wa shughuli za chama hicho kitaifa.


0 Comments