LIBYA KUFANYA UCHAGUZI

Viongozi walioambatana na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya umepongeza zoezi hilo la uchaguzi wa kwanza wa mabaraza ya miji nchini Libya katika mwaka huu wa 2021 na kusifu irada na azma ya kitaifa ya nchi hiyo katika kutumia haki zake za kidemokrasia.

Mazungumzo ya kutafuta amani ya kudumu nchini Libya na kuitisha uchaguzi wa rais kwa shabaha ya kuhamisha madaraka kwa njia za kidemokrasia yanaendelea huku nchi hiyo ikiendelea kusumbuliwa na uingiliaji wa madola ya kigeni katika masuala ya ndani ya nchi hiyo. 

Misri na Uturuki zinatambuliwa kuwa wachezaji wakuu katika medani ya siasa za ndani za Libya na katika wiki za hivi karibuni zimezidisha harakati zao nchini humo. 

Wiki kadhaa zilizopita Bunge la Uturuki lilirefusha muda wa majukumu ya jeshi la nchi hiyo huko Libya kwa kipindi kingine cha miezi 18. 

Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya inayoungwa mkono na Uturuki imeimarisha zaidi jeshi lake katika medani ya vita ya Sirte-Al Jufrah. 

Safari ya maafisa wa ngazi za juu wa jeshi la Uturuki nchini Libya, upinzani wa jenerali muasi, Khalifa Haftar dhidi ya safari hiyo na sisitizo lake la kushambuliwa wanajeshi wa Uturuki, vilevile masharti yake kwa ajili ya kuondoka Libya wanajeshi hao, vimeendeleza mgogoro wa ndani wa Libya licha ya mazungumzo yanayofanyika sasa baina ya makundi hasimu.

Hata hivyo kufanyika uchaguzi wa mabaraza ya miji nchini Libya katika mazingira ya sasa kunatambuliwa kuwa ni tukio zuri na chanya na kielelezo cha irada na azma ya makundi mengi ya kisiasa na wananchi wa Libya kwa ujumla kwa ajili ya kuijenga upya nchi hiyo na kuanza kipindi kipya katika nchi hiyo iliyoharibiwa na vita.

Post a Comment

0 Comments