QATAR YAONDOLEWA VIKWAZO.

Saudi Arabia itaondoa zuio la muda mrefu kwa Qatar ya kufunga anga na mipaka ya ardhi na bahari dhidi ya Qatar iliyodumu kwa takriban miaka mitatu.

Waziri wa Mambo ya nje wa Kuwait Ahmad Nasser al-Sabah alitangaza makubaliano hayo kwenye Televisheni ya Kuwait Jumatatu, akisema "Makubaliano yamefikiwa kufungua anga na mipaka ya ardhi na bahari kati ya Saudi Arabia na Qatar kuanzia jioni hii.

Alisema makubaliano hayo yatasainiwa katika mkutano wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba (GCC) huko Saudi Arabia Jumanne.

Mfalme wa Saudi Arabia Salman ndiye atakayeongoza mkutano huo na kiongozi wa Qatar anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo kwa mara ya kwanza tangu mipaka ilipofungwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita.

Mzozo wa kidiplomasia ulianza mnamo mwaka 2017 wakati Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, Bahrain na Misri zilipokata uhusiano wa kidiplomasia, biashara na usafiri na Qatar.

Nchi hizo nne zilishutumu Qatar kwa kuunga mkono ugaidi.

Post a Comment

0 Comments