MATOKEO KIDATO CHA SITA COASTAL HIGH SCHOOL YANG'ARA MKOA WA TANGA


Mwalimu wa Taaluma Coastal High School Isaack Dastan Kikwete



Shule ya Sekondari Coastal High iliyopo Chumbageni mkoani Tanga imeendelea kun'gara kwenye matokeo ya kidato cha sita ya Mwaka 2020/2021 baada ya Wanafunzi kuwa na ufaulu wa Daraja la Kwanza na Pili tu (Division I na II)yaliyopatikana shuleni hapo na kuifanya kuwa ya kwanza katika wilaya ya Tanga.

Hayo yamebainishwa na  Mwalimu wa Taaluma wa shule hiyo Isaack Dastan Kikwete ambaye amesema siri kubwa ni walimu kujituma na kuwapa wanafunzi lengo la shule pindi anapoingia shuleni hapo.

"Kwa mwaka 2020/2021  tumefanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha sita,kwa wanafunzi wetu kupata daraja la kwanza nala Pili pekee(Division I na II)tumeendelea kuwa shule ya kwanza(Namba 1)katika wilaya ya Tanga mjini na tumekuwa shule ya nne(Namba 4) kwa mkoa wa Tanga"alisema Kikwete

Aidha Mwalimu Kikwete amesema mafanikio hayo hayakuja tu,ila yamechagizwa na uongozi pamoja na walimu walio bora ikiwemo kujituma bila kuchoka na wanafunzi kuwa na ari katika masomo.

"Kwanza ni ushirikiano kutoka kwa Mkurugenzi Mathew Marupa,kuwa na walimu bora na wanajitoa kwa muda wote,bidii kwenye masomo wanayosimamia pamoja na kuwa na wanafunzi wanaojitambua ambapo pale wanapofika wanapewa malengo ya shule kuwa hautakiwi kufeli unapokua kwenye shule hii"alisema Kikwete.

Hata hivyo ameeleza kuwa kwa miaka minne mfululizo,shule imeendelea kufanya vizuri kwa kuwa wanafunzi wanakuwa katika mazingira bora ya kujifunza

"Kwenye mchakato wa elimu ushirikiano ni muhimu,tunaamini mafanikio ya elimu ni ushirikiano wa walimu na wafanyakazi wengine ambao sio walimu "alisema Kikwete.

Post a Comment

0 Comments