Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa ya G7
********
Viongozi wa kundi la mataifa saba yaliyoendelea kiuchumi duniani ya G7watajumuika mchana wa 13.12.2024 katika kutafuta muongozo wa pamoja kwa serikali mpya ya Syria, ambayo imeahidi kulinda utawala wa sheria baada ya miaka mingi ya dhuluma chini ya rais aliyepinduliwa Bashar al-Assad.
Assad aliikimbia Syria baada ya mashambulizi makali yaliyoongozwa na kundi la Kiislamu la Hayat Tahrir al-Sham (HTS) na washirika wake, ambayo yalimaliza ghafla miongo mitano ya utawala kandamizi wa ukoo wake.
Viongozi hao wa Kundi la Mataifa Saba ambayo pia yana nguvu za kidemokrasia, watafanya mkutano kwa njia ya mtandao wamesema wako tayari kuunga mkono kipindi cha mpito kwa kile wanachokisema kuundwa serikali "jumuishi na isiyo ya kidini" nchini Syria.
Mataifa ya G7 yataka kuwajibishwa kwa utawala wa Assad kwa tuhuma za uhalifu ingawa tayari walitoa wito wa kulindwa kwa haki za binadamu, zikiwemo za wanawake na walio wachache,huku wakisisitiza umuhimu wa kuuwajibisha utawala wa Assad kwa uhalifu wake.
0 Comments