RUSSIA YASHAMBULIA MIUNDO MBINU YA UMEME

Urusi imefanya mashambulizi makubwa kwenye vituo vya nishati vya Ukraine, Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati wa Ukraine Galushchenko. Mashambulizi hayo yanafanyika wakati Ukraine ikiendelea kutoa mwito kwa washirika wake wa kupatiwa mifumo zaidi ya ulinzi wa anga.

Akitumia mtandao wa Facebook,Waziri wa Nishati wa Ukraine,Galushchenkoamesema kwa mara nyingine adui yao Urusi ameendeleza mashambulizi ya kutisha. Sekta nzima ya nishati ya Ukraine inakabiliwa na mashambulizi makubwa.

Mifumo ya nishati ya Ukraine tayari ilikuwa imeshambuliwa kwa mara ya kumi na moja na Urusi mwaka huu pekee na mashambulizi hayo yamesababisha uharibifu mkubwa na kukatika kwa umeme kwa muda mrefu kote nchini humo.

Kwa mujibu wa shirika la nishati la Ukraine,  Ukrenergo ni kwamba hata shambulizi la leo Ijumaa  limepelekea baadhi ya watu nchini humo kukosa huduma ya umeme.

Usiku wa kuamkia leo kelele za mifumo ya ulinzi wa anga zilishamiri katika maeneo mengi ya Ukraine kuashiria mashambulizi ya anga.

Baadaye mamlaka ziliripoti kutokea kwa milipuko mingi katika eneo la kusini mwa mji wa Odesa na katika maeneo ya mji mkuu Kyiv ambapo mifumo hiyo ya ulinzi wa anga ilikuwa ikifanya kazi.

Post a Comment

0 Comments