Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran ameashiria matukio ya Syria na kusema muqawama utaimarika na kuwatimua waliovamia ardhi ya Syria na kuikalia kwa mabavu.
Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami Khatibu na Imamu wa Swala ya Ijumaa wiki hii mjini Tehran amesema kinara wa kundi hili,ambayo ameibuka,alisema wazi kwamba hana nia ya kuanzisha vita dhidi ya Israel.
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran amesema inajulikana vyemba kwamba a vyema kwamba kinara wa kundi hilo lililonyakua Madaraka Syria ni kibaraka wa utawala wa Kizayuni na kwamba utawala wa Kizayuni ulimsaidia.
"Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, nchi za eneo na Saudi Arabia, Misri na Jordan kwa uwazi kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel umechukua fursa ya hali iliyojitokeza kuikalia zaidi Syria na kuharibu miundombinu yote ya nchi hiyo."
Amesema lengo la utawala wa Kigeni ni kunyakua ardhi zote za nchi za Kiarabu kutoka Mto Nile hadi Mto Euphrates amesema utawala wa Kigeni ni ukiimarika utazifuata nchi hizo za Kiarabu na hivyo zinapaswa.
Aidha amesema kwa miaka 45 sasa tokea Mapinduzi ya Kiislamu yapate ushindi nchini Iran maadui wamejaribu kutekeleza kila aina ya njama dhidi ya nchi hii lakini wamefeli.
0 Comments