Moja ya Darasa lililokabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulidi Surumbu,hafla iliyofanyika katika kijiji cha Mazola.
Mratibu wa Worldvision Tanzania katika wilaya ya Mkinga Evodia Shija akiwa na Mkuu wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulidi Surumbu kwenye uzinduzi wa choo cha Wanafunzi.MKUU wa Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga Kanal Maulid SulumbuMratibu wa Worldvision Mkinga Evodia Shija Wanachi waliojitokeza wakifuatilia kwa ukaribu shughuli zinavyoendelea Mazola.
*******************
MKUU wa Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga Kanal Maulid
Sulumbu amepokea miradi ya zaidi ya Millioni 800 kutoka shirika la Worldvision Tanzania.
Kanali Maulid Sulumbu amesema kukabidhiwa kwa miradi 18 ya madarasa,afya, maji,lishe na usafi wa mazingira miradi ambayo imegarimu zaidi ya
shilingi milioni 800.
Kanali
Sulumbu amelishukuru shirika la World vision kwa kutoa kiasi hicho cha
fedha kwa ajili ya kutatua changamoto zinazoikabili jamii kwenye wilaya
hiyo jambo ambalo wadau wengine wa maendeleo wanapaswa kuliiga.
"Mchango
wao ni mkubwa kwa kuwa umeweza kuchangia upungufu wa madarasa tulio nao
katika shule za msingi wameweza kutupunguzia adha ile ya kuwa na
upungufu wa madarasa zaidi ya 2000 na sasa ivi tunazungumzia upungufu wa
madarasa 1500 na wako tayari kuendelea kutusaidia kwenye sekta hii pale
ambapo watapata uwezo"alisisitiza Kanal Sulumbu.
Aidha Kanali Sulumbu amesema Wilaya ya Mkinga ni miongoni mwa Wilaya za Mkoa
Tanga ambazo zilipata upungufu wa chakula ikiwemo Wilaya ya Handeni na
Mkinga ambapo mwaka jana shirika hilo liliweza kupeleka chakula
mashuleni jambo ambalo limekwenda kuongeza ufaulu.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Elizabeth Dickson amesema miradi
inakwenda kuwanufaisha wana Mkinga hivyo wao kama Halmashauri wapo
tayari kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ili
kuhakikisha adhma ya serikali ya kuwahudumia wananchi kwa kutoa huduma
bora na zenye hadhi inayotakiwa kulingana na kauli mbiu ya mheshimiwa
Rais wao kama Halmashauri wanaitimiza na kuitekeleza ipasavyo.
"Kwetu
sisi ni faraja kuwepo kwa miradi hii kwanza inakwenda kuongeza ufaulu
kwa watoto lakini pia inakwenda kuimarusha afya za watoto kupitia
vyakula wanavyovipata mashuleni pia uhakika wa usalama wa maji vile vile
miradi hii inakwenda kuongeza tija kwa wananchi na kupunguza kiwango
cha utoro kwa wanafunzi hivyo kwetu kama Halmashauri ni faida kubwa
sana, "alisema Kaimu Mkurugenzi.
Mratibu
wa Worldvision Mkinga Evodia Shija amesema miradi hiyo inalenga kuweka
mazingira rafiki kwenye sekta ya elimu, maji na afya.
Evodia
amesema kuwa shirika hilo la Worldvision linafanya kazi katika maeneo
yote bila kujali dini, kabila wala ubaguzi wa aina yeyote ile hivyo
wanashirikiana na serikali kuboresha miundombinu ambayo inamfanya mtoto
aweze kuishi kwa furaha.
"Miradi
ya leo tuliyokabidhi ni 18 ikiwemo vyoo, madarasa, zahanati, mradi
wa umwagiliaji lengo tunataka kuboresha mazingira ya jamii zetu kwa
kuwasaidia kuondokana na adha mbalimbali zinazowakabili katika maeneo
yao, "alisema Evodia.
Wanafunzi
wa shule ya msingi Mazola akiwemo Asha Hassan na Mohamed Omari
wameonesha furaha yao kupata madarasa matano yanayokwenda kuwaondolea
adha ya kukaa chini pamoja na kuondoa utoro kwa wanafunzi shuleni hapo.
Miradi
hiyo 18 yenye zaidi ya shilingi milioni 800 imetekelezwa na shirika
hilo kwenye Wilaya hiyo ya Mkinga na kwamba uhitaji huo pia unaonekana
kwenye tarafa nyingine zilizopo kwenye wilaya hiyo jambo ambalo wadau
wa maendeleo wanapaswa kuliunga mkono.





0 Comments